Haendi Popote, Ten Hag Kumzuia Onana AFCON

 

Haendi Popote, Ten Hag Kumzuia Onana AFCON

MANCHESTER United ipo kwenye mazungumzo na mamlaka ya soka ya Cameroon ili kumzuia Andre Onana asishiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).


Kipa huyo wa mashetani wekundu anahofia huenda akapoteza nafasi yake kikosi cha kwanza endapo atakosa mechi sita za Ligi Kuu England akiwa katika majukumu ya kimataifa, kuanzia Januari 11 hadi Februari 13.


Sheria za mashindano zinasema, atapigwa marufuku kuichezea klabu yake endapo atakataa kujiunga na timu ya taifa ya Cameroon kwa ajili ya fainali hizo.


Lakini kocha Erik ten Hag alisema: “Onana akiitwa timu ya taifa ataenda. Lakini tupo kwenye mazungumzo.”


Onana alistaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kuzozana na kocha wa Cameroon, Rigobert Song jambo ambalo limemfanya kujiondoa wakati wa fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar mwaka jana.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alimalizana na kocha wake wa taifa ambaye aliwahi kuichezea Liverpool kuanzia mwaka 1999 na 2001.


Endapo Cameroon itamjumuisha Onana kwenye kikosi anaruhusiwa kuandika maombi kwa shirikisho la soka la taifa hilo, ili kuepuka adhabu kutoka FIFA. Kwa mujibu wa sheria ndogo ya FIFA inasema mchezaji akigoma atazuiwa kuichezea klabu yake.


kwa mujibu wa Ten Hag anataka Onana abaki Old Trafford kwani anaamini ni mmoja wa makipa bora zaidi duniani akiwa na umri wa miaka 27.


Onana alikosolewa kutokana na makosa yake iliyogharimu timu yake kuambulia sare ya mabao 3-3 dhidi ya 3-3 dhidi ya Galatasaray Jijini Istanbul Jumatano usiku katika michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya.



Lakini kocha wake amemtetea akidai: “Ukichambua vizuri basi unaona ni kipa wa pili kwa ubora Ligi Kuu England kwa kuzingatia takwimu. Anaendelea vizuri kwenye ligi, lakini anatambua alifanya makosa, kumbukeni katika miaka mitano amefanya vizuri Ligi Mabingwa Ulaya msimu uliopita, ana uzoefu mkubwa tangu alipokuwa Ajax na Inter Milan.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad