Haroub Canavaro Awafungukia Yanga 'Inabidi Wabadilike, Ukiangalia Kwa Haraka ni Kama Safari Yao Umefika Mwisho Ligi ya Mabingwa'


Nadir Haroub ‘Canavaro’ Kuhusu Yanga Ligi ya Mabingwa
Nadir Haroub ‘Canavaro’ Kuhusu Yanga Ligi ya Mabingwa

Nahodha na beki wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’ amesema wachezaji wa Yanga wazingatie HESHIMA, Utulivu na Kujitoa wawapo uwanjani kucheza na timu kubwa hasa zinazoshiriki michuano hiyo mikubwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Ukiangalia kwa haraka uwaweza kusema safari ndo imefika mwisho, kutokana na aina ya uchezaji wa wachezaji wa Yanga, wanapaswa kubadilika wakiwa wanacheza na timu kubwa hasa mashindano haya.“

“Ni kuzingatia heshima kwa maana ya kumheshimu mpinzani wako, utulivu na kujitoa binafsi, timu kama Mediama sio wa mchezo mchezo, wanapaswa kujipanga,” alisema Canavaro ambaye pia amewahi kuwa mchezaji wa Taifa Stars na meneja wa timu hiyo.

Kuhusu uzoefu wa wachezaji wa Yanga kwenye michuano hiyo, Canavaro alisema; “Yanga ni timu kubwa, sisi tuliwafunga hapo hapo kwa Mkapa, hivyo uzoefu isiwe sababu.” Ikumbukwe kuwa, Machi 2014, Yanga iliifunga Al Ahly bao 1-0 kwenye uwanja huo na michuano hiyo hiyo, bao pekee la Yanga lilifungwa na Canavaro dakika ya 83 akifunga kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Simon Msuva.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad