Jeshi la Polisi la Mtia Mbaroni Mtuhumiwa Aliyemuua Beatrice Minja



Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Beatrice James Minja ambayo aliyafanya huko Tarekea Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjro Tarehe 12.11.2023 na mtuhumiwa aliyefanya aliyefanya tukio hilo kukimbia.

Akitoa taarifa hiyo leo kwa vyombo vya Habari Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi lilianza mara moja uchunguzi kumtafuta aliyefanya tukio hilo ambapo mapema leo Disemba 31.12.2023 Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa Lukas Paul Tarimo.

SACP Misime amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa mafichoni huko Kijiji cha Jema kata ya Olondonyosambu Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Aidha amebainisha kuwa baada ya Mtuhumiwa kuhisi atafikiwa na Mkono wa sheria alijaribu kunywa sumu ya kuua wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo mtuhumiwa huyo na jitihada za kumkimbiza katika kituo cha afya zilifanyika ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri huku akisubili taratibu za kisheria.

Pia Msemaj wa Jeshi hilo amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na Jeshi la Polisi kitendo kilichopelekea mtuhumiwa wa mauaji kukamatwa huku akiwaomba wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad