Kiemba Afichua Kwa nini Penalti ya Simba ilirudiwa

 

Kiemba Afichua Kwa nini Penalti ya Simba ilirudiwa

Mchambuzi wa soka Amri Kiemba, ameainisha kwa nini penalti kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Kagera iliyochezwa jana katika Uwanja wa Uhuru ilirudiwa.


Amesema kurudiwa kwa penalti kunatokana na sababu hizi hapa;


“Penati inaweza kurudiwa ikiwa kipa atatoka kwenye mstari kwa sababu alifaidika na makosa yake,lakini pia inaweza kurudiwa ikiwa wachezaji wanaohusika kuzuia watawahi kuingia kwenye 18 hayo yote yataangaliwa ikiwa itakoswa”


“Lakini pia penati inaweza kurudiwa ikiwa timu inayohusika kufunga wataingia kwenye 18 kabla ya mpigaji kupiga ,kwanini mmeingia na mmefunga ? kwa hiyo itarudiwa”


“Tukio la leo watu wametazama kama kosa la golikipa kwa sababu aliyeitisha hilo tukio (kibendera) anahusika moja kwa moja kuangalia kama kipa atatoka kwenye mstari”


“Lakini ukiangalia wachezaji wa timu zote mbili waliingia na mkiingia wote nyie mnaozuia ndio mtaadhibiwa” Kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, Simba iliibuka na ushindi wa 3-0 likiwemo goli hilo lililofungwa baada ya penalti kurudiwa baada ya ile ya awali ambayo kipa aliicheza, ilionekana kulikuwa na hayo makosa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad