Kocha Mamelodi Ajibu Kauli ya Mayele Kunyimwa Visa Kuingia South Afrika

 

Kocha Mamelodi Ajibu Kauli ya Mayele Kunyimwa Visa Kuingia South Afrika

Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rulani Mokwena amejibu tuhuma za mshambuliaji wa Pyramids FC, Fiston Mayele kuwa alinyimwa viza ya kuingilia Afrika Kusini wiki mbili zilizopita akidai hazikuwa za kweli.


Mokwena amejibu tuhuma hizo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Pyramids, juzi huko Misri.


Katika mchezo wa kwanza baina yao ambao ulifanyika Afrika Kusini, Mamelodi ililazimishwa sare tasa kama huo lakini Mayele hakuwa miongoni mwa wachezaji wa Pyramids waliosafiri kwenda Afrika Kusini kutokana na kukosa Viza ya kuingia nchini humo.


Kwa mujibu wa mtandao wa idiskitimes.co.za wa Afrika Kusini, Mokwena alisema kuwa Mamelodi isingeweza kufanya jambo kama hilo kwa vile sio la kiuanamichezo.


"Hatuchezi mechi kwenye Twitter, mechi haichezwi kwenye Twitter, inachezwa katika eneo la kuchezea na ninaweza kukuambia ninatoka katika nchi ambayo unakuwa huna hatia hadi pale itakapobainika una hatia na kwake kutoa tuhuma kama hizo ni kutoitendea haki klabu yetu.


"Sisi ni klabu inayoongozwa na maadili, ukweli na usawa na tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuwa klabu ya namna hiyo ndani na nje ya eneo la kuchezea," alisema Mokwena.


Ikumbukwe Mayele aliilalamikia Mamelodi kuwa imemfanyia figisu akose Viza wakati timu yake ilipokwenda kukabiliana nao.


"Sawa mmekataa kunipa viza mkiamini mtatufunga subutu. Pointi moja muhimu sasa tukutane Cairo," alinukuliwa Fiston Mayele.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad