Papa Francis amewaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsi moja, yakiwa ni maendeleo makubwa kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja na mahusiano mengine ya kijinsia wanaofahamika kama LGBT katika Kanisa Katoliki la Roma.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki la Roma amesema makasisi wanapaswa kuruhusiwa kuwabariki wapenzi wa jinsi moja na wanandoa “isiyo ya kawaida”, kwa misingi ya hali fulani.
Lakini Vatican ilisema baraka hazipaswi kuwa sehemu ya taratibu za kawaida za Kanisa au zinazohusiana na miungano ya kiraia au harusi.
Iliongeza kuwa inaendelea kuiona ndoa kuwa kati ya mwanamume na mwanamke.