Mama Mazazi wa mtoto Sabrina Abdallah (9) aliyefariki dunia Desemba 6, baada ya kuteleza na kuzama kwenye maji mengi ya Mto Morogoro, amefungua mazito kifo cha mwanaye.
Akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi jana Bi Hellena Abdallah Maarufu Mama Sabrina alieleza A-Z tukio hilo lililoondoa uhai wa Mwanae.
”Ilikuwa Desemba 6 majira ya saa 8 mchana mpendwa mwanangu Sabrina alitoka shuleni nikamuandalia chakula, alipomaliza kula mvua ikanyesha, mimi na yeye tukatoka nje kukinga maji ya mvua, ilipotaka mimi na Sabrina tukaingiza ndoo hizo za maji ndani.
"Wazazi wangu wanaishi Chamwino, juzikati alikuja Prinsess ambaye ni mtoto wa ndugu yangu, rika lake ni kama Sabrina, baada ya mvua kukata wakaniaga kwamba wanakwenda kucheza na dada yake huyo mgeni. Kama unavyoona nyumba yetu ipo jirani kabisa na mto.
"Sabrina alimuambia dada yake huyo mgeni waenda mtoni kutazama maji yamejaa. Walipofika mwanangu aliteleza na kusombwa na maji, nikiwa ndani naongea na simu Prinsess alikuja huku akilia na kuniambia Sabrina ametumbukia mtoni nikakimbia kuelekea mtoni, nilipofika sikumuona mwanangu, jinsi maji yalivyokuwa mengi sikuamini kama mwanangu atakuwa hai.
"Watu wakaingia majini kumtafuta baada ya lisaa hivi namuona nwanangu analetwa na boda boda akiwa tayari amefariki Dunia,” alimalizia kusema Mama Sabrina na kuangua kilio.
Naye Maneno Shabani ambaye ni fundi selemara katika mtaa huo akizungumza na Mtandao huu alisema.
”Jana sikulala nimeweweseka usiku kucha, ntoto Sabrina alikuwa akicheza hapa na wenzie baada ya muda nasikia amesombwa na maji wakati tunatafakari hilo nimeshuhudia anapitishwa hapa akiwa amepakatwa na Juma Vigogo kwenye bodaboda.
"Shigo yake ililegea leges na tumbo lilikuwa limejaa maji akiwa tayari amefariki, nilishindwa kujizuia nakaangua kilio,” alisema Fundi huyo.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa River Side, Kata ya Mwembesongo, Manispaa ya Morogoro, Hashimu Bito, alisema;
”Baada ya kupata taarifa nilipiga simu Faya, walifika na kuzama kwenye maji wakimtafuta mtoto huyo bila mafanikio, wakati Maafande wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kumtafuta eneo hilo, mkazi wa hapa Mtaa Juma Vigogo alisema kutokana na kasi ya maji, huenda mtoto huyo akawa amesombwa kwenda mbali zaidi.
"Juma aliwaacha Maafande wa Faya wakiendelea kumtafuta hapo Top Ten yeye kambia kuelekea bondeni alipofika Daraja la Kichangani kuna watu wanaosha Pikipiki na Magari pembezoni ya daraja hilo, wakamueleza muda huu tumeona mguu wa mtoto ukielea juu ya maji.
"Taarifa hizo zilimtia moyo kakimbia hadi daraja la Mafisa Mzambarauni barabara kuu ya Moro-Dar baada ya kama dakika 5 kamuona Sabrina anapita kazama kwenye maji kamuopoa.
"Baada ya kumuopoa Kakodi Boda boda kampakata na kuja naye hapa akamkabidhi kwa Maafande wa Faya, wakati anazama kwenye Maji viatu vya Juma Kigogo vilisombwa na Maji kaja hapa akiwa Pekupeku,” alisema Mwenyekiti huyo.
Akihojiwa kwa njia ya simu leo Asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
lfahamike Kutoka eneo aliliozama Mtoto huyo nyuma ya baa ya Top Ten mpaka daraja la Mzambarani ni takribani umbali wa Mita elfu Mbili kwa maana ya Viwanja 20 vya Mpira wa Miguu.
Kufuatia taarifa hizo Mwandishi wa Mtandao huu amemtafuta Muokoaji huyo Juma Vigogo ambaye hana mafunzo yoyote ya Uokoaji na kueleza mbinu alizotumia kumpata Mtoto huyo.