Mama wa Chid Benz afunguka ishu ya mwanae

  

Mama wa Chid Benz afunguka ishu ya mwanae

Mama wa Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro, Chid Benz ameonesha kushangazwa na tabia za mwanaye huyo kutoacha matumizi ya dawa za kulevya licha ya kusaidiwa na kupatiwa matibabu mara kwa mara.


Hivi karibuni ilisambaa video ya Chid Benz akiomba pesa mtaani lakini hali yake ilionekana imedhoofika huku baadhi ya watu wakidai kuwa muonekano huo wa King Kong unaashiria amerejea tena kwenye urahibu wa dawa za kulevya.


"Baba mzazi wa Chid alikuwa meneja wa Shirika la Nyumba pale Ilala. Sasa mimi nilikuwa naenda kuulizia nyumba katika kwenda pale tukakutana, tukapendana akanioa.


"Mtoto huyu nimemuuguza kwa muda mrefu na katika maisha yangu sikutegemea nitakuwa na mtoto kama hivi anavuta unga na nini maana kama ni kusaidiwa amesaidiwa na watu kibao.


"Kusikia mwanao kabebwa huku, kabebwa kule mtu hutegemei unaipata tu. Kijana alikuwa mzuri, anaimba vizuri, anafanya kazi vizuri hata Mhe. Mwigulu Nchemba alikuja hapa tukakaa hapahapa kwa ajili ya Chid," amesema katika mahojiano na Clouds TV.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad