Marehemu Nisher Alikuwa Mtu Mwenye Vipaji Vingii...



Mwongozaji maarufu wa video za muziki nchini, Nic Davie 'Nisher' ambaye ni mtoto wa Muhubiri GeorDavie wa jijini Arusha amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 12, kwa mujibu wa taarifa ya familia yake ambayo haikutaja chanzo.

Nisher, 38 alitambulika na wengi kama director wa video za muziki lakini katika tasnia alionyesha talanta zake nyingine kama uimbaji na utayarishaji wa muziki, huku ndipo hasa alianzia. Kulingana na taarifa kutoka kwenye tovuti yake, Nisher alivutiwa kuingia kwenye sanaa na mwimbaji wa Marekani, Usher Raymond kuanzia mwaka 2000, mnamo 2005 akasafi kwenda nchini humo kujifunza muziki na kurusha vipindi vya televisheni.

Kupitia mtandao wa Instagram familia ya GeorDavie imetangaza kifo cha Nisher na kusema msiba unafanyika katika nyumba ya matamko Kisongo Jijini Arusha.

"Familia ya Nabii Mkuu, Dk Geordavie inasikitika kutangaza kifo cha kijana wao mpendwa, Nic Davie (Nisher) kilichotokea usiku wa kuamkia leo, saa nane na dakika tisa. Msiba unafanyika katika nyumba ya matamko Kisongo Jijini Arusha, Tanzania," imeeleza taarifa iliyotolewa na familia.


Ikumbukwe video ya wimbo wa Joh Makini, Sijutii (2012) akimshirikisha Dunga iliyofanyika jijini Arusha ndio ilimtangaza zaidi Nisher na kuanza kufanya kazi za wasanii mbalimbali hasa wa Bongofleva.

Miongoni mwa video alizoongoza Nisher ni ‘Listen’ ya Belle 9, ‘Press Play’ ya DJ Choka, ‘Maktaba’ ya Bonta, ‘Mama Yeyoo’ ya G Nako, ‘Dole’ ya Mabeste, ‘Jikubali’ ya Ben Pol, ‘Kijukuu’ ya Young Dee, ‘Bila Wewe’ ya Jordan, ‘2030’ ya Roma, ‘Nakomaa na Jiji’ ya Shilole.

Nyingine ni ‘Nje ya Box’ ya Nikki wa Pili, ‘XO’ ya Joh Makini, ‘Amani ya Moyo’ ya Feza Kessy, ‘Arosto’ ya G Nako, ‘Baby’ ya Mirror, ‘Unanichora’ ya Ben Pol, ‘13’ ya Young Killer, ‘Bongo Hip Hop’ ya Fid Q, ‘Wayu Wayu’ ya Dogo Janja, ‘Homa’ ya Lulu Diva n.k.

Mwaka 2014 marehemu Nisher alishinda Tuzo za Watu kama Muongozaji wa Video Anayependwa akiwashinda Adam Juma na Hanscana ambao aliingia nao fainali.

Nisher pia amewahi kutayarisha muziki miongoni mwa nyimbo alizotengeneza ni pamoja na ‘Bendera ya Chuma’ ya Fid Q uliyochezwa Coke Studio Africa, na ‘Amani ya Moyo’ wake Feza Kessy ambao nao ulichezwa Big Brother Africa.

Pia aliingia studio na kurekodi nyimbo zake kama ‘So Fresh’ na ‘Rapper’, vilevile alisikika kwenye wimbo 'My Time' uliokutanisha wasanii kama Gentriz, Dogo Janja, M-Rap, Climax na Country Boy.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad