Meneja wa Msanii wa Muziki #Phina , @d_fighter1 ameonesha kutokupendezwa na kauli alizozitoa Meneja mkongwe wa Tasnia ya Muziki @mkubwafellatmk kwenye moja ya mahojiano yake akizungumzia kuhusiana na Tuzo #TMA katika kipengele cha Meneja bora ambapo Tuzo hiyo aliichukua #Dfighter na #Fella kusema tuzo hiyo ilipelekwa kwa mtu ambae ni Underground.
Kupitia kurasa wake wa Instagram #Dfigher amefunguka kuwa #MkubwaFella amemkosea na kuikosea taasisi iliyoandaa Tuzo na amekikosea kiwanda chetu cha burudani:
Ameandika haya:
Wahenga hawakukosea waliposema samaki ana mengi ya kuongea lakini mdomoni maji.
Juzi nilipigiwa simu nyingi sana na wadau na wapenzi wa sanaa waliofuatilia mahojiano ya meneja mkongwe mkubwa fella katika kituo kimoja cha radio, katika mahojiano hayo mkubwa aliteleza maana kiheshima wanasema mkubwa hakosei, alisikika akibeza mimi kupewa Tuzo kama meneja bora na kuona sikustahili kuibeba kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Tuzo za muziki Tanzania, yote tisa kumi mkubwa akaonyesha hata kutojua jina langu na pia kuonyesha watangazaji wasinijue.
Bila kupepesa macho na bila kuvunja heshima ya wakubwa wetu ni wazi mkubwa alikosea sana, alinikosea binafsi, ameikosea taasisi iliyoandaa Tuzo na amekikosea kiwanda chetu cha burudani. Naomba hapa nimkumbushe kuwa mimi sio manager underground kama alivyoniita , kutokuwa kwenye generation yake hakunifanyi niwe underground maana nimewasimamia wasanii wengi kabla ya hawa wanaovuma sasa hivi ukianzia kwa Mesen Selekta, Pam D, Ray C ndio nikaja kumtoa Marioo kuanzia wimbo wa kwanza hadi sasa anafanya vizuri na hata Phina nimemchukua wimbo wa kwanza hadi leo anafanya vyema kwenye kiwanda.
Wasanii wote niliowasimamia wamefanya mambo makubwa ikiwemo kushiriki Tuzo za ndani na za kimataifa bila kuwepo kwenye LABEL yoyote , je mkubwa bado ni underground wakati tunakutana na wasanii wa LABEL yenu kwenye matuzo na madilj huko au hatutakiwi kukua mbele ya macho yenu.
Tumekuwa tukipokea kejeli na vijembe vingi na kauli za kuonyesha tunabebwa bebwa au hatustahili tupatacho, tumekaa kimya muda mrefu ila kwa sasa hapana maji yamepungua mdomoni wacha tuseme.Manatuchukia bure wakati familia zenu zinajirekodi nyimbo zetu, mafurikon hayawezi zuiwa kwa mkono na kila jambo lina nyakati yake na huu ni wakati wetu KUBALINI tu.
Tunajua mnapenda nyimbo zetu and tutaendelea kutoa nyimbo nzuri na tutaendelea kuchukua Tuzo maana #SISINIWALE na kubwa tunza heshima yetu ili nasi tutunze ya kwako. Ukubwa ni dhamana usitumike vibaya