Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, Janeth Mayanja akitolea ufafanuzi kuhusu Hali ya mafuriko yaliyotokana na vua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini ambapo mvua hizo zinatajwa kunyesha tangu usiku wa kuamkia Leo.
Mlima Hanang unatajwa kuelemewa na kwa mvua hizo na sehemu ya Mlima huo kuporomoshwa na Mvua baada ya kulegea udongo katika sehemu ya Mlima Hanang na kupelekea mawe na udogo ulioambatana na vua hadi kwenye sehemu ya makazi ya watu wilayani humo.
“Leo asubuhi tumepata changamoto hapa Hanang toka jana usiku zilikuwa zikinyesha mvua za kawaida lakini maji yakawa yameporomoka kutoka Mlima Hanang yakiwa na mawe na miti kuja katika Mji wa Kateshi yakiwa na nguvu.
"Mpaka sasa tumepata vifo vya watu 47 pamoja na majeruhi ambapo maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Tumaini lakini pia uharibifu wa miundombinu ya barabara kati ya Sindiga na Babati yamesimama kwa muda ila TANROADs na TARURA wapo hapa kuhakikisha mawasiliano yanarejea.
“Pia niwaombe Wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati jitihada za uokoaji zikiendelea,” amesema DC Janeth.