Kufuatia taarifa ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kueleza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) imemsimamisha kazi Mwalimu Japhet Maganga kwa tuhuma za utoro kazini, Maganga amejibu ana haki ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa mujibu wa Katiba ya CWT Ibara ya 30 (e) Toleo la Mwaka 2014 huku akidai ana mkataba wa kudumu wa ajira ya chama hicho
Maganga ambaye anatuhumiwa pia kukaidi maelekezo ya viongozi wake amesema “Niliajiriwa #CWT kama Mhasibu Januari 1, 2018, niligombea Ukatibu Mkuu nikitokea Idara ya Uhasibu CWT-Makao Makuu na si Halmashauri, hivyo nina haki ya kuendelea kushika nafasi hiyo.”
Ikumbukwe Januari 25, 2023, Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya lakini hawakwenda kuapa, baadaye Maganga alitakiwa kurejea kituo chake cha kazi (Shule ya Msingi Tandika - Temeke) ikielezwa nafasi yake CWT ilikuwa ya kuzimwa kwa kibali maalum ambacho muda wake ulimalizika Septemba 30, 2020