Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limetoa ufafanuzi juu ya taarifa za Mwanamke mmoja wa miaka 40 Mkazi wa Kazegunga ambaye anadaiwa kuonekana November mwaka huu baada ya kufariki October 17,2018 wakati akijifungua Mtoto katika Hospitali ya Baptist iliyopo Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji na kuzikwa Kazegunga alipokua kaiishi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Filemon Makungu amesema kuna matukio mawili ya Watu ambao wameonekana wakiwa hai ingawa Familia wamesema walifariki “Matukio haya tumeyafatilia yote na inatakiwa kuthibitisha kisayansi tumeshapeleka vipimo kwa Mkemia Mkuu bado hatujaletewa majibu tukiletewa tutatoa maelezo yaliyokamilika lakini kwa matukio haya mawili bado upelelezi tunaendelea nao kujua kwa kina zaidi ili kujua ukweli wa yule aliyefariki na huyu aliyeokotwa akiwa hai”
Mwezi November mwaka huu Familia ilisema Mpendwa wao huyo alionekana katika eneo la Ilagala Wilayani Uvinza ambapo miezi 11 iliyopita tukio kama hili la Mtu kufariki kisha kuzikwa na kuonekana tena lilitokea Kijiji cha Kandaga Wilayani UVinza Mkoani Kigoma ambapo pia mazingira yake yanahusishwa na imani za kishirikina kutumika kupoteza Watu na kuonekana tena baada ya muda mrefu kupita.
Mpaka sasa imeshawahi kuripoti matukio matano kama haya ya kusemekana Mtu amefariki na kuzikwa na baadaye Ndugu kudai wamemuona tena Ndugu yako akiwa hai, matukio hayo yametokwa mwaka 2018 Kasulu, mwaka 2020 Kasulu, mwaka 2021 Kasulu, mwaka 2022 Uvinza na mwaka 2023 Kigoma DC.