Nafasi ya Pili yaikera Yanga, Wadai Wao ni wa Namba Moja tu

Nafasi ya Pili yaikera Yanga, Wadai Wao ni wa Namba Moja tu
 

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuna uwezekano wa kumaliza mwaka ikiwa nafasi ya pili kutokana na uwezekano wa kutomaliza baadhi ya viporo vya timu hiyo.


Kamwe ameyasema hayo jijini Dodoma leo Ijumaa, Desemba 22, 2023 kabla ya mchezo Yanga dhidi ya Tabora United ambao watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini hapa kuanzia saa 1:00 usiku.


Katika michezo 10 iliyocheza Yanga kwa sasa katika Ligi Kuu, timu hiyo tayari imefanikiwa kuvuna jumla ya pointi 27 ikisaliwa na mechi tatu ukiwamo unaopigwa kesho dhidi ya Tabora, huku nyingine mbili zikiahirishwa tena na Bodi ya Ligi (TPLB) kupisha mchezo wa kirafiki wa timu za taifa, Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes.


Mechi hiyo itakayotumika kuzindua uwanja wa Amaan uliokuwa unatengenezwa, uitapigwa Desemba 27 siku moja kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024. Michezo ambayo Yanga bado haijacheza ni michezo dhidi ya


Tabora United unaopigwa kesho pamoja na ile ya Kagera Sugar uliokuwa upigwe Desemba 26 na mwingine wa Mashujaa Kigoma wa Desemba 29 ambao yote imetangazwa kuahirishwa na Bodi hadi baada ya fainali za Afcon 2023 zinazofanyikia Ivory Coast.


"Kwenye ratiba ambayo tupo nayo tuna mechi na Tabora, lakini pia ratiba ilikuwa inaonyesha tuna mechi na Kagera, Mashujaa lakini nafikiri kwa muingiliano wa mashindano mbalimbali ambayo yamekuja nafikiri kuna michezo tunaweza tusiweze kuikamilisha kabla ya mwaka kuisha" aliongeza Kamwe.


Kwa sasa msimamo wa Ligi unaongozwa na Azam iliyokusanya pointi 31 baada ya kucheza michezo 13, huku ikifuatiwa na Yanga na Simba ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 na leo inashuka uwanjani kucheza mchezo wa 10 ikiivaa KMC.


Kamwe amesema kuahirishwa kwa mechi hiyo kunaifanya Yanga hata ikishinda kesho dhidi ya Tabora United, itafikisha pointi 30, moja pungufu na ilizonazo Azam na hivyo kuifanya iuage mwaka 2023 ikiwa nafsi hiyo ya pili.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad