Ostaz Juma: Manara na Zaylissa Wanatangaza Ufuska na Uasherati wa zinaa

Ostaz Juma: Manara na Zaylissa Wanatangaza Ufuska na Uasherati wa zinaa

 

Ostaz Juma aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi la Watanashati amewatolea uvivu haji Sunday Manara na aliyekuwa mke wa msanii Dullah Makabila maarufu kama Zaylissa baada ya wawili hao kudaiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.


Manara na Zaylissa wamekuwa wakijiachia pamoja katika maeneo mbalimbali ya starehe si mchana tu mpaka usku na hata kusafiri pamoja, pia zipo baadhi ya video clip zikiwaonyesha wakiwa nyumbani kwa Manara.


"Naomba kujua zaidi kuhusu hawa watu. Hawa watu walipokutana kwenye party na kupata mvinyo ndio chanzo cha haya yote. Je, kila moja alikua hana mpenzi kabla ya siku hiyo?


"Ina maana hawakua kwenye mahusiano ya kimapenzi kabisa? Ama wamewasaliti wapenzi wao? Na kama wamewasaliti wapenzi wao je, unahisi kwamba ni wakweli kwenye mahusiano? Au ndio kuueneza ufuska na uasherati wa zinaa nakuutangaza mitandaoni.


"Tuachane na Manara ambae alikwenda kufanya umra makka na kumlilia mungu amsamehe makosa yake kisha alipo rudi tunashuhudi wenyewe anayo yafanya ambayo hayakubaliki hata kidogo.


"Je, huyu bidada pia hakua na mpenzi kweli ama ndio alipo kwenda kwenye party ndio chanzo cha kuachana na mpenzi wake!? Mbona sielewi kila ninavyo fikiria zaidi napata jibu baya kila nikiwaza napata jibu baya.


"Pamoja na yote, kweli nimeamini simba akikosa nyama anakula nyasi bado na bado sana bidada hamfikii hata kidogo Rushaynah," ameandika Ostaz Juma.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad