Polisi: Mlioibiwa Simu, TV fikeni 'Sentro' kutambua mali zenu

 

Polisi: Mlioibiwa Simu, TV fikeni 'Sentro' kutambua mali zenu

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amewataka wananchi walioibiwa simu na vifaa vingine vya kielektroniki kama vile runinga, kompyuta na redio kufika katika kituo cha polisi cha Sentro kwa ajili ya kuzitambua mali zao.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 19, 2023 kituoni hapo, Muliro amesema mali hizo zimekamatwa katika oparesheni maalum iliyoanza Septemba ambapo wamefanikiwa kuwakamata wahalifu 27.


"Watu waje kuzitambua mali zao. Tumekamata kompyuta mpakato 10, Simu za mkononi 305, runinga 36, makava ya simu 160, kamera 4 na redio (subwoofer) 3, amesema Muliro.


Amesema tayari baadhi ya mali hizo zimeshatambuliwa na hatua za kuwashughulikia wahalifu kwa mujibu wa sheria zinaendelea

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad