Polisi yatoa tamko tuhuma za utesaji wa raia

 

Polisi yatoa tamko tuhuma za utesaji wa raia

Baada ya shutuma kuelekezwa katika Jeshi la Polisi nchini, zilizotolewa na Wananchi wawili katika nyakati tofauti na habari zao kusambaa katika mitandao ya kijamii wakidai kubambikiwa kesi kukamata na kuteswa kinyume cha sheria, Jeshi hilo limenzisha uchunguzi wa malalamiko hayo.


Kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisi ya Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, imeeleza kuwa mitandao miwili tofauti ya kijamii, zilionekana taarifa za Wananchi wakilalamika kufanyiwa vitendo vilivyo kinyume cha haki za binadamu na baadhi ya Askari Polisi.


Jeshi la Polisi limeeleza kuwa limeziona video za malalamiko hayo na limeanza uchunguzi kwa kushirikisha wataalam wengine wa haki jinai, kuchunguza malalamiko hayo, huku likitaka wenye ushahidi kulingana na malalamiko yalivyowasilishwa na walalamikaji asisite kujitokeza ili ukamilike mapema na hatua nyingine za kisheria zifuate.


Kauli hii inakuja siku moja baada ya taarifa kuhusu kunyanyaswa kwa baadhi ya raia akiwemo Mkazi wa Dodoma, Kalamba Mnenge anayedai kukamatwa na hatimaye kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Nkuhungu Mjini Dodoma, ambapo aliteswa na kudhalilishwa huku Getrude Masanja alilalamika kufanyiwa visivyo huko Mkoani Kilimanjaro.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad