Sababu ya Wasani wa Tanzania kuachwa kwenye Rolling Stone Top 40 Best Afro-Pop

 

Sababu ya Wasani wa Tanzania kuachwa kwenye Rolling Stone Top 40 Best Afro-Pop


Sababu ya Wasani wa Tanzania kuachwa kwenye Rolling Stone Top 40 Best Afro-Pop


Umekuwa utamaduni wa jarida la Rolling Stone kuchapisha orodha ya nyimbo 40 bora za Afro-pop kila mwaka.


Orodha ya nyimbo 40 za mwaka 2022 ilihusisha wimbo wa Marioo X Jovial – Mi amor, ambao ulikuwa namba 39; na wimbo pekee kutoka Tanzania.


Mwaka huu, orodha hiyo haijataja wimbo wa msanii kutoka Tanzania, licha ya wasanii wa Bongo Fleva kufanya nyimbo nyingi zilizoacha alama kubwa mwaka huu.


Kwanini Wasanii wa Tanzania hawajatokea kwenye orodha?


Rolling Stone hawatumii waandishi na wachangiaji wa kitanzania wanapokusanya taarifa zao. Wachambuzi wa muziki wanaotoa maoni yao kwenye jukwaa hilo, sio raia wa Tanzania. Mara nyingi makala hizo zinaandikwa na waandishi raia wa Kenya, Nigeria, Afrika Kusini na Ghana, ambao wanatumia nafasi hiyo kutangaza zaidi utamaduni wao.


Sababu pekee kwanini @marioo_tz alionekana kwenye orodha hiyo, ni kolabo na Jovial, Mkenya aliyekuwa anawakilisha nchi ya mwandishi aliyeandika aya yake. Mwandishi huyo alikosea jina la wimbo na kumfanya Jovial kuwa mmiliki namba moja. (Jovial X Marioo, badala ya Marioo X @jovial_ke), na Marioo alishukuru bila kumkosoa mwandishi kwa kumnyima haki yake, kwani aliyezungumziwa zaidi kwenye aya hiyo, alikuwa Jovial wala sio Marioo.


Wasanii wetu wengi wanasimamia kazi zao binafsi, hawawezi kukamilisha kila kitu kinachotakiwa kufanya ikiwemo kuhakikisha kazi zao zinahifadhiwa kwenye kumbukumbu za vyombo vingi vya habari.


Muziki wa Tanzania unakosa sifa zake ughaibuni kwa sababu wachambuzi wake wa muziki hawapati nafasi kwenye majukwaa ya kidigitali. Gharama za kuendesha majukwaa ya kidigitali bado ni kubwa, kitu kinachofanya kuwa na idadi ndogo ya wachangiaji wenye muendelezo.


Makala hii ni wito kwa wawekezaji kwenye kiwanda cha muziki na majukwaa ya kidigitali; kusaidia kupata wataalam wanaoweza kuungwa mkono na kufanikisha kuutangaza utamaduni wa Tanzania kwa kuandika na kutunza rekodi nyingi za wasanii na taarifa zilizogusa maisha ya mashabiki wa Bongo Fleva.


Na, @enkyfrank

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad