Sare Zashikilia Matumaini ya Wananchi Ligi ya Mabingwa, Msimamo wa Kundi D Huu Hapa

 

Sare Zashikilia Matumaini ya Wananchi Ligi ya Mabingwa, Msimamo wa Kundi D Huu Hapa

Matokeo ya sare katika mechi mbili za Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika zilizochezwa jana, yamefufu ndoto za Yanga kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano hayo, licha ya kutoka sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Medeama leo.


Ukiondoa mechi hiyo ya Yanga ambayo imemalizika kwa sare jana Desema 8, 2023; kwenye Uwanja wa Baba Yara, Kumasi, Ghana, mchezo mwingine wa kundi hilo ulikuwa ni baina ya Al Ahly iliyoialika CR Belouizdad ambao ulimalizika kwa sare tasa.


Katika mchezo dhidi ya Medeama jana, Yanga ilisubiri hadi dakika ya 36 kusawazisha bao la Medeama kupitia kwa Pacome Zouzoua aliyefunga kwa shuti la wastani la mguu wa kushoto mpira ambao alipora kwa mchezaji wa Medeama.


Kabla ya hapo, wenyeji walitangulia kupata bao katika dakika ya 27 kupitia kwa Sowah Jonathan kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa na refa Ibrahim Mutaz kutoka Libya baada ya Dickson Job kumuangusha Daniel Lomotey katika eneo la hatari.


Matokeo ya jana yamefanya Yanga ifikishe pointi mbili katika kundi hilo nyuma ya Al Ahly yenye pointi tano zikifuatiwa na Medeama na CR Belouizdad ambazo kila moja ina pointi nne.


Kwa namna msimamo wa kundi ulivyo, kama Yanga itapata ushindi katika mechi mbili zijazo nyumbani dhidi ya Medeama na Belouizdad, itafikisha pointi nane ambazo zinaweza kuisogeza hadi nafasi ya pili au ya kwanza kutegemea na matokeo ya mechi nyingine ambazo zitakutanisha Al Ahly na Belouizdad na Medeama.


Pamoja na hilo, Yanga imeshindwa kuvunja mwiko wa Medeama kupoteza mechi za kimataifa nyumbani ambapo kwa sare ya jana, timu hiyo ya Ghana imefikisha mechi ya 14 bila kupoteza, ikishinda mechi 12 na kutoka sare mbili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad