Simba Wataja Dau la Chama Endapo Timu Itamtaka, Yanga Watajwa





Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba.
KAMA Yanga wapo siriazi kumsajili kiungo mchezeshaji Mzambia, Clatous Chama wapo watoe dau la dola 300,000 (zaidi ya Sh 752 Mil) ili waununue mkataba wake wa mwaka mmoja ambao ameubakisha Simba.

Tetesi zinasema kuwa kiungo huyo, anawaniwa vikali na baadhi ya klabu za hapa nchini kati ya hizo ni Yanga ambaye anatajwa kwenda huko na Azam FC.

Kiungo huyo hivi karibuni alisimamishwa na uongozi wa Simba kutokana na utovu wa nidhamu pamoja na kiraka Nassoro Kapama ambao hawapo kambini hivi sasa.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Simba imekubali kumuachia kiungo huyo kwa sharti la timu husika inayomuhitaji kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja kwa dau hilo la zaidi ya Sh 700Mil.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, uongozi wa Simba hauna utamaduni wa kumzuia mchezaji kuondoka hapo na kwenda sehemu yenye maslahi yake.


Clatous Chama
Aliongeza kuwa wanaheshimu ubora wa kiungo huyo mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao, lakini kama mwenyewe akihitaji kuondoka hapo, kamwe hawatamzuia kikubwa afuate taratibu na aheshimu mkataba wake.

“Ili mkataba wa Chama uvunjwe, basi klabu husika itatakiwa kutumia zaidi ya Sh 700Mil, kama kikitoka kiwango hicho cha fedha, basi uongozi hautamzuia kuondoka hapo.

“Kiwango hicho fedha kipo katika mkataba wake Chama, ili timu itakayomuhitaji kumsajili iwe ndani au nje ya nchi, basi itatakiwa kutoa dau hilo la fedha.

“Kama kiwango hicho cha fedha kitatoka, basi hatutamzuia mchezaji huyo kuondpoka, kwani hiyo fedha itakayopatikana kutokana na mauzo yake yatamsajili mchezaji mwingine wa kiwango chake,” alisema mtoa taarifa huyo.

Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, hivi karibuni alizungumzia hilo la usajili kwa kusema kuwa “Hatima ya mchezaji kuachwa au kuuzwa lipo chini ya kocha wetu Benchikha (Abdelhak) ambaye yeye ndiyo atatoa mapendekezo ya usajili, kwani yeye ndiye anajua umuhimu wa kila mchezaji katika timu.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad