Klabu ya Simba inaonekana imeanza kurejesha makali yake taratibu haswa kwenye ligi ya mabingwa Afrika ambapo walionekana kuanza vibaya zaidi msimu huu kuliko misimu mingine ya hivi karibuni.
Wekundu wa Msimbazi walianza michuano ya ligi ya mabingwa Afrika kwa mguu wa kushoto msimu huu, Kwani mpaka kufikia michezo mitatu walikua hawajapata ushindi katika mchezo wowote ambapo walipata sare michezo miwili na kufungwa mchezo mmoja.
Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako.
Tunasema klabu hiyo inarejea kwenye ubora wake kwasababu ilifanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza kwenye ligi ya mabingwa Afrika ambapo walipata ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya klabu ya Wydad Casablanca kutoka nchini Morocco.
Baada ya ujio wa kocha Benchikha ameonekana kuibadilisha klabu hiyo kwa kiwango kikubwa licha ya kukaa kipindi kifupi ndani ya timu hiyo, Hivo wengi wanatarajia makubwa kutoka kwa kocha huyo mkubwa barani Afrika.
Matumaini ambayo yalionekana kufifia kwa klabu ya Simba kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika yameonekana kufufuka upya, Hii ni baada ya ushindi dhidi ya Wydad Casablanca ambao umewatoa mkiani kwenye kundi D na kuwapeleka mpaka nafasi ya pili wakiwa na alama 5.
Klabu ya Simba imejiwekea malengo ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika jambo ambalo wamekua wakilipigania kwa misimu takribani mitatu sasa, Japo msimu huu ilionekana kama wasingeweza kufuzu hata hatua ya robo fainali lakini ujio wa kocha Benchikha umeibua matumaini upya