Taarifa Kuhusu Mtanzania Mwigine Aliyeuawa Huku Israel na Hamas



Serikali ya Tanzania imethibitisha kupokea taarifa kutoka serikali ya Israel kuhusu kifo cha mwanafunzi Joshua Mollel aliyekuwa anasoma nchini Israel na aliyetekwa nyara tarehe 7 Oktoba 2023 wakati kundi la Hamas liliposhambulia Israel.


Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba amesema ameongea Mzee Mollel kuhusu ujumbe huo.


‘Tunaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel, kuungana na Balozi wetu na maafisa waliopo huko, kukutana na kuzungumza na mamlaka za nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada. Kwa ridhaa ya familia, na itakapobidi, tutatoa taarifa za ziada katika siku zijazo’.


Joshua ni mwanafunzi wa pili kutoka Tanzania ambaye kifo chake kimethibitishwa kufuatia shambulio hilo la Hamas baada ya kile cha Clemence Mtenga ambaye pia alikuwa Israel kwa masomo ya Kilimo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad