No title



Tajiri wa timu ya TP Mazembe, Moise Katumbi yamemkuta mapya baada ya kuzuiwa kusafiri kwenda kutazama dabi ya watani kati ya timu yake na FC Lupopo inayopigwa leo.

Muda mfupi ujao Mazembe itashuka uwanjani kumenyana na Lupopo mechi itakayochezwa Jiji la Kalemie ukihamishwa kutoka Jiji la Lubumbashi ikihofiwa mchezo huo kuweza kuleta ghasia kubwa kutokana na upinzani wa timu zote mbili.

Katumbi ambaye ni mmoja wa wagombea wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo amefika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Lubumbashi maarufu kwa Luano tayari kwa safari na kukutana na zuio hilo.

Bilionea huyo amekutana na taarifa ya mamlaka ya anga kuwa ndege yake binafsi imekosa kibali cha kutua Jiji la  Kalemie hatua ambayo itamfanya kuikosa mechi hiyo.

Inaelezwa mbali na kuhofia machafuko ya vurugu zinazoweza kutokea baina ya mashabiki wa klabu hizo mbili kulikuwa na kila dalili za Katumbi kuzuiwa kwenda Jiji la Kalemie kutokana na mgombea huyo kuanza kulalamikia mchakato wa uchaguzi huo unasubiriwa kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.

Mapema wiki hii Katumbi amesikika akikosoa mchakato wa uchaguzi wa nchi hiyo akidai mambo mengi hatakwenda kwa usafi katika kuondoa udanganyifu wa  matokeo hayo ambayo mpaka Sasa mpinzani wake mkubwa rais Felix Tshekedi anayeongoza kwa mbali
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad