Tanesco Wajibu Kauli ya Paul Makonda Kuhusu Kuwepo Kwa Watendaji Wazembe


Tanesco Wajibu Kauli ya Paul Makonda Kuhusu Kuwepo Kwa Watendaji Wazembe

Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kenneth Boymanda amesema wamepokea kauli iliyotolewa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda kuhusu Shirika hilo na tayari wameanza kuyafanyia kazi kikamilifu maelekezo yaliyotolewa.

Akiongea na @AyoTV_, Boymanda amesema “Ndani ya Shirika tunayo sera ya upimaji ufanisi wa kazi kwa Watendaji na kama kuna changamoto za kiutendaji kwa Watumishi wa Shirika hilo, hatua stahiki zinachukuliwa kwa wote ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na ubora unaotakiwa”

“Niwaombe sana Wananchi watuvumilie kwenye kipindi hiki ambacho uzalishaji haukidhi mahitaji, Shirika linafanya kila jitihada kuhakikisha kipindi hiki tunakipita salama wakati tukisubiria mashine ya kwanza katika mradi wa Bwawa la Nyerere”

Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam jana pamoja na mambo mengine Makonda alinukuliwa akiwaambia TANESCO “Je maumivu, mzigo na shauku anayoibeba Rais Samia ndio hayohayo Watendaji wa Tanesco wanayabeba ama wanamuachia Mwenyekiti wetu peke yake ? ukiona hadi Rais anavunja bodi maana yake hili suala halivumiliki, tunawauliza Watendaji wa Tanesco mnajiona mnastahili kweli kumuwakilisha Rais Samia ama mnasubiri tenda, anavunja bodi, atengue, ateue....... huku hamumtendei haki Rais Samia, kuna vingine ni uzembe tu, unapokaa ofisini na kutoa maelezo ofisini bila kwenda site mnatengeneza picha tofauti”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad