KOCHA Mkuu wa Manchester United, Eric Ten Hag amewapa moyo mashabiki wa timu hiyo kuwa kundi kubwa la majeruhi wa timu wakipona basi wana nafasi ya kufanya vizuri.
Kauli hiyo ameitoa Ten Hag baada ya kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya West Ham katika mchezo wa Ligi Kuu England na kuifanya timu hiyo kumaliza mwaka 2023 vibaya kwa kichapo.
Ten Hag akizungumza baada ya mchezo huo alisema: “Hatukuwa tumewapa kitu wapinzani wetu (West Ham) hadi dakika 72 ambapo kila kitu kilibadilika. Kila mtu hapa United anatakiwa kuwajibika.
“Tunatakiwa kuwa wapole na kukaa pamoja, kusimamia mpango wetu na kuufanya kwa pamoja na kuwa wapole tena.
“Kwa mwaka 2023 tulishinda ubingwa, tukacheza fainali ya FA na tukawa watatu kwenye ligi. Hizo zilikuwa nyakati nzuri ila sasa tunacheza chini ya kiwango.
“Lakini kuna sababu – tuna majeruhi wengi, tutakuwa vizuri pale watakaporejea. Sasa tunatakiwa wamoja.”