Timu ya Simba Hawamtaki Kabisa Chama?

 

Clatous Chotta Chama

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.


Taarifa zinasema kuwa klabu ya Simba haitamuongezea mkataba nyota huyo pindi mkataba wake wa sasa utakapofikia tamati mwezi June mwaka 2024, kutokana na mahitaji ya klabu hiyo kuwa makubwa kuliko uwezo wa mchezaji.


Chama amekuwa na wakati mzuri tangu alipojiunga na klabu ya Simba mwaka 2018 akitokea Lusaka Dynamo ya kwao nchini Zambia, akiiwezesha Simba kushiriki Ligi ya mabingwa Barani Afrika hatua ya robo fainali na kubeba mataji ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara pamoja na kombe la shirikisho [FA].


Chama amebeba mataji matatu [3] akiwa na Simba, kabla ya kuondoka kwenda RS Berkane na kisha kurejea tena.


Mchezo wake wa kwanza baada ya kujiunga na Simba ilikuwa dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ilikuwa 20/09/2018 walipopoteza kwa goli 1-0.


Goli lake la kwanza aliifunga klabu ya Stand United ya Shinyanga katika uwanja wa Benjamin Mkapa, 21/10/2018 wakati klabu yake ikiibuka na ushindi wa goli 3-0.


Aidha klabu hiyo ipo kwenye mpango wa kufanya usajili mkubwa mapema mwezi June utakaoiwezesha klabu hiyo kutoa ushindani wa kutosha kutoka ndani ya Tanzania na kwenye Ligi ya mabingwa Barani Afrika.


Tayari baadhi ya majina ya nyota wenye uwezo mkubwa yameshawekwa mezani kuelekea dirisha kubwa la usajili la mwezi June 2024

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad