Uchaguzi Chipukizi CCM wakosolewa
Hakuna dhambi yeyote ya watoto hao kugombea nafasi na kupata, changamoto kuna watoto wengi ambao hawawezi kupata taarifa sahihi na wazazi wao hawana uelewa mpana wa masuala ya siasa, kwahiyo kunaonekana watu wale wale kupeana madaraka
Dk Loisulie alisema tafsiri iliyoibua mjadala ni tabaka linalotawala kujiimarisha kuendelea kubaki madarakani jambo ambalo ni wasiwasi ambao unaeleweka.
“Wale ambao hawajabahatika kuingia kwenye nafasi za uongozi hawatakaa kusogelea nafasi za uongozi ndio wasiwasi uliopo,” alisema Kwa upande wake msaikolojia John Amrose alisema siasa nisuala la kijamii hivyo hakuna shida mtoto kujihusisha nayo.
“Siasa ni suala la kijamii ambalo mtu anakuzwa nayo kwa kujua malengo, utendaji na wajibu,jambo linaloleta shida ni wale tunaowaona wanazaliwa na viongozi waliopo madarakani ambalo kisaikoolojia ikunakuzwa kuona uongozi si kwa jamii yetu bali ni kwa mtoto wa fulani, kunakuwa kama ufalme wenye mihimili fulani, “Kwahiyo otukiwa na chipukizi wanaotokana na viongozi ambao tayari wapo madarakani ni shida kubwa kwa baadae,” alisema.