Uchambuzi Mechi ya Simba na KMC, Simba Ufanisi Ulikuwa Mdogo, KMC Game Bora Sana


Simba na 4-2-3-1 kama kawaida yao , walianza mchezo wakiwa chini sana : wanafanya makosa mengi hasa wakishambulia (wanapoteza pasi kirahisi , movements zao hazikuwa sahihi , hawakuwa na maamuzi ya pasi za mwisho + ufanisi ulikuwa mdogo .

Kmc na mikakati ya kuzuia kwanza then washambulie kwa kushtukiza : Nafikiri ndio ulikuwa mtego wao sahihi hasa mbele ya Simba , Walifanikiwa hasa kipindi cha kwanza ( wakipora mipira wanaunda mshambulizi kwa haraka “Counter Attacks” walichokosa ni ufanisi na maamuzi . DECISION MAKING . Kwa kipindi cha kwanza Kmc wangeweza kuondoka hata na goli zaidi ya moja .

Kipindi cha pili , Simba waliongeza ufanisi mbele ya goli , walifanya vitu vya kimsingi sana : Pasi sahihi , Movements , Ufanisi . 2-4-3-1 wakati Simba wanashambulia (Saido Kibu na Mzamiru nyuma ya Baleke then Zimbwe na Kapombe mstari mmoja na wale viungo wawili Ngoma na Kanoutè ) waliwaruhusu FBs kusogea juu zaidi + Kibu anaingia kwenye “Half Spaces” na Mzamiru mda mwingi alicheza ndani kwenye kiungo . Simba walitengeneza idadi kubwa ya wachezaji wakati wanashambulia .

Nafikiri kama Kmc wangekuwa na maamuzi sahihi kwenye eneo la mwisho basi walikuwa na nafasi ya kuimaliza game mapema kipindi cha pili . Kuna nyakati ni wao tu kuweka mpira kwenye nyavu ( Elias , Awesu , Makang’a Wazir Jr walikosa maamuzi wakifika kwenye eneo la mwisho .

NOTE:

Wazir Jr kwenye nyakati sahihi ✅

Wale Kmc wakiwa na mali 👏🔥 Watulivu sana ✅ Awesu , Ibrahim Elias 🔥

Maseke amecheza game bora👏 …. Kapombe ✅ Kibu D anaubonda sana aisee 🔥

FT: Kmc 2-2 Simba

By Kevinrabson

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad