Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kutoka Lugalo limefanikiwa kuokoa wafanyakazi wa Kampuni binafsi ya uendeshaji mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) Jijini Dar es salaam (UDART) waliokua wamekwama katika ofisi hizo zilizopo Jangwani Jijini hapa.
Akizungumza na ManaraTv leo wakati zoezi la uokoaji likiendelea Inspector Helman Edwin kutoka Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji amesema mpaka sasa wamefanikiwa kuokoa wafanyakazi nane na bado zoezi la uokoaji linaendelea.
Aidha ameongoza kuwa mpaka sasa hukuna majeruhi wala vifo na kuwataka wafanyakazi hao kuchukua tahadhari wakati huu ambapo mvua zinaendelea kunyesha.