Wakija mashoga, wasagaji siwezi kuwabariki - Askofu Ruwai'chi

 


Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam Jude Thaddaeus Ruwai'chi ametoa wito kwa Jamii hususani waumini wa Kanisa hilo kuwa wafuatilie kwa makini tamko lililotolewa hivi karibuni na na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis na kuepuka uzushi wa mitandaoni huku wakibaki na uelewa na msingi wa mafundisho sahihi ya Kanisa Katoliki.


Akizungumzia mjadala ulioibuka hivi karibuni unaodai kuwa Papa Francis amebariki Ndoa za Jinsia moja Askofu Ruwai'chi ameeleza kuwa tamko la Baba Mtakatifu limehusu Baraka, Baraka ambazo mtu yeyote anaweza kuomba isipokuwa yule anayeomba Baraka hizo asiwe na mategemeo ambayo yanakinzana na msimamo na misingi ya Kanisa lakini pia hawapaswi kutengwa au kuuwawa kama baadhi ya nchi zinavyofanya ila wanakaribishwa kutubu na kumrudia Mungu- Papa Francis


Amesema bahati mbaya iliyopo ni kwamba Mazingira ambayo mafundisho ya Baba Mtakatifu Yametolewa kuhusu hiyo Baraka yametekwa na Watu kwenye Jamii na kwenye mitandao ambao kimsingi hawalitakii mema Kanisa Katoliki


"Kimsingi akija mtu kwangu kwa mfano akisema naomba Baraka, sifahamu kama ni Shoga au sio Shoga mimi nitambariki lakini endapo wanakuja Watu wawili wananiambia Sisi ni Mashoga tunaomba utubariki nitawauliza ninyi niwabariki katika lipi?, na nitashindwa kuwabariki katika Ushoga wao nitawashauri, nitawaelekeza kutafuta namna ya kukabili changamoto yao na kutubu lakini kanisa haliwezi kubariki dhambi na mimi kama mimi sitaweza kuwabariki katika misimamo na mielekeo ya Kishoga isipokuwa wanakaribishwa kutubu na kumrudia Mungu."


Ameendelea kusisitiza kuwa hakuna Baraka yoyote ambayo itatengua mafundisho ya msingi kuhusu ndoa ambapo ndoa ya Wakatoliki ni muunganiko kati ya Mume na Mke na muunganiko huo ufanyike katika nia iliyo sahihi na si kinyume cha hapo kwa kuwa ndoa inalenga kushirikiana na Mungu katika kazi ya uumbaji.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad