Yanga wanahitaji hiki tu kusinda mechi zao na kwenda Robo Fainali

 

Yanga wanahitaji hiki tu kusinda mechi zao na kwenda Robo Fainali

Matokeo ya suluhu iliyoipata Al Ahly nyumbani Cairo dhidi ya CR Belouizdad yameifanya Yanga kuwa na matumaini ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Yanga ilipata sare ya bao 1-1 na Medeama ya Ghana mchezo wa tatu wa kundi D na kufikisha pointi mbili ikisalia nafasi ya mwisho kwenye msimao.


Matokeo ya ushindi kwenye mechi mbili zijazo dhidi ya Medeama na CR Belouizdad kwenye Uwanja wa Mkapa na angalau sare dhidi ya Al Ahly ugenini, itaifanya Yanga kufikisha pointi tisa na hivyo kujihakikishia nafasi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu Afrika.


Hadi sasa vinara Al Ahly na Yanga zimetofautiana pointi tatu, wamisri hao wakiwa nazo tano na Yanga tatu na matumaini ya Wanajangwani kufuzu ni kushinda mecho zake mbili za nyumbani na sare au ushindi ugenini dhidi ya Al Ahly ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa michuano hiyo.


Al Ahly, Medeama na CR Belouizdad zitakutana zenyewe kwa zenyewe na kuweka uwezekano wa kutibuliana kabla ya Yanga kwenda kumaliza kampeni zao za msimu huu ugenini cairo dhidi Misri ambayo ilitoka naye sare ya 1-1 Kwa Mkapa.


Yanga imeonyesha inazimudu timu ilizocheza nazo licha ya kutopata ushindi, ikimaanisha inahitaji nidhamu zaidi ili kuzimaliza zikija Kwa Mkapa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad