Yanga yaanza na Wakenya, Simba yapewa Jamuhuri Mapinduzi Cup



 

Yanga yaanza na Wakenya, Simba yapewa Jamuhuri Mapinduzi Cup

Kamati ya mashindano ya Kombe la Mapin-duzi kwa mwaka 2023 imetoa ratiba yote ya mashindano hayo, huku wababe wa soka la Tanzania Yanga na Simba wakifunga na kufungua mwaka 2023 na 2024 mtawalia.


Kombe la Mapinduzi litaanza Desemba 28, 2023 kwenye Uwanja wa Amaan uliofanyiwa ukarabati mkubwa na kuwa wa kisasa.


Mabingwa watetezi Mlandege watafungua mashindano hayo kwa kucheza na URA SC ya Uganda saa 10:15 jioni na baadaye Azam FC, mabingwa mara tano wa Kombe la Mapinduzi watakuwa wageni wa Chipukizi kutoka kisi-wani Pemba, mchezo ambao utachezwa kuanzia saa 2:15 usiku.


Yanga SC itashuka dimbani Desemba 31 ku-wakaribisha Bandari ya Kenya saa 2:15 usiku, wakati Singida Fountain Gate watacheza na APR ya Rwanda Januari 1, 2023.


Simba SC, mabingwa mara nne wa Mapinduzi Cup watashuka dimbani kuvaana na Jamhuri kutoka Pemba Januari 1, 2023 saa 2:15 usiku.


Michezo yote hiyo utachezwa kwenye Uwan-ja wa Amaan na mchezo pekee ambao una-tarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Gombani kule kisiwani Pemba ni wa nusu fainali ya kwanza ambayo utamkutanisha mshindi wa robo fainali ya kwanza dhidi ya yule wa robo fainali ya pili utakaochezwa Januari 10, 2023.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad