Yanga Yaifanyia Umafia Simba Yamsajili wa kiungo Mkabaji wa JKU



UMAFIA! Ndiyo utakavyoweza kusema ni baada ya mabosi wa Yanga kuwazidi ujanja Simba, baada ya kufanikisha usajili wa kiungo mkabaji kinda wa JKU, Shekhan Hamis, 18.

Hiyo ni katika kuelekea dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa leo kwa timu kuboresha vikosi vyao kutokana na mapendekezo ya kocha ambayo ameyapendekeza.

Tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Muargentina Miguel Gamondi ametoa mapekezo ya wachezaji ambao anawahitaji katika kukiboresha kikosi chake katika dirisha dogo.

Mmoja wa Mabosi wa Yanga ameliambia Championi Ijumaa kuwa, Makamu wa Rais wa timu hiyo, Arafat Haji ndiye aliyekamilisha dili hilo la usajili kwa kiungo ambaye anakuja kuwa mbadala wa Mganda, Khalid Aucho.


Bosi huyo alisema kuwa, Simba waliku wa kwanza kumfuata kiungo huyo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kumsajili kabisa ambapo walimtuma mmoja wa viongozi wao huko Unguja visiwani Zanzibar lakini baada ya Yanga kupata taarifa haraka wakamtumia Arafat ambaye anafaya kazi huko kukamilisha usajili.

Aliongeza kuwa Yanga wamefanikisha usajili huo kwa dau la Sh 60Mil, akisaini mkataba wa miaka mitatu huku akilipwa kwa mafungu, tayari nyota huyo amemtanguliziwa Sh 20Mil.

“Tumefanikisha usajili wa kiungo mpya Shekhan ambaye anakuja kuwa mbadala wa Aucho, tumeingia mkataba wa miaka miwili kwa dau la Shilingi 60Mil tukiwa tumemtangulizia 20Mil.


“Tumefanikisha dili hilo la usajili baada ya vita kubwa ya usajili iliyokuwepo kati yetu na Simba, vita hiyo tumeishinda kwa kishindo kwa kumsajili Shekhan mkataba wa miaka mitatu,” alisema bosi huyo.

Yanga bado inaendelea na usajili wa wachezaji wake katika dirisha dogo, ambao wamepanga kusajili wachezaji wanne kati ya hao yupo kiungo mkabaji, winga na mshambuliaji.

Alipotafutwa  Katibu Mkuu wa JKU  ya Visiwani Zanzibar, Shadhil Khatib alisema nyota huyo kwa sasa sio mali yao baada ya kukamilisha usajili na klabu ya Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Amesema kwa upande wao wamemalizana na Yanga baada ya makubaliano ya uhamisho wa kiungo huyo ambaye ukifika muda Yanga watamtambulisha.

“Ni kweli kwa sasa Shekhan sio mchezaji wetu kwa sababu amesaini mkataba wa miaka mitatu na tumeshamalizana na Yamga kuhusu uhamisho wa nyoya wetu huyo,” amesema katibu huyo.

Shekhan ni moja ya viungo bora vinana wanachipukia kwa sasa ndani ya soka la visiwani Zanzibar, mwenye ubunifu mkubwa akiwa uwanjani na ni moja ya viungo wenye mashuti makali sana.

Stori na Wilbert Molandi na Ibrahim Mussa

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad