Yasemekana Hii Ndio Sababu ya Mchezaji Chama Kusimamishwa Simba


Yasemekana Hii Ndio Sababu ya Mchezaji Chama Kusimamishwa Simba

Kabla ya kuanza kwa mechi ya Simba dhidi ya Wydad Casablanca juzi pale Benjamin William Mkapa wakati wa kufanya Mazoezi ya kupasha misuli Chama alipewa maelekezo ya program ya Mazoezi na mwalimu wa viungo Kamali kisha Chama akaonekana kutokukubaliana na hilo wakarushiana maneno na chama akapiga mpira chini kuonyesha kuchukizwa na hilo, mwalimu Selemani Matola alimfata Chama na kumtuliza aachane na hicho kinachoendelea huku beki Henock Innonga alikwenda kumtuliza Mwalimu wa Viungo kamali juu ya jambo hilo kisha baada ya mchezo kutamatika Mwalimu wa Viungo Kamali akaamua atoe ripoti hiyo kwa kocha mkuu Abdelhak Benchikha naye Benchikha akalifikisha hilo swala kwenye uongozi wa Simba na hatimaye limetolewa maamuzi hayo ya kusimamishwa na kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu na maadili.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad