Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,
Albert Chalamila amesema kuna baadhi ya Watu wamegeuza ulemavu kuwa mtaji kwa kuwatuma Walemavu kuomba barabarani kisha pesa wanazichukua wao ambapo kufuatia hali hiyo ameagiza Walemavu wote wanaoomba barabarani wakamatwe na wapelekwe kwenye vituo vya kulelea Walemavu.

“Kwakweli Mtaa hauzai, wanaoita Watoto wa mitaani ni kukwepa jukumu la kumuita Mtoto wa Juma, hakuna Mtaa unaojifungua hakuna, kwahiyo agizo langu kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya wa Dar es salaam kuna Watu wanazagaazagaa kwenye maeneo ya msingi kwa mfano Tanzanite Bridge ukienda pale Ubungo fukuzeni wote, na hasa kwa mfano wale Walemavu kamateni wanaoendesha kwenye vile vibaiskeli ambao wanaomba kama wale”
“Tumethibitisha ni miradi ya walio sio Walemavu, wale ambao sio Walemavu wamekusanya Walemavu wanawatembeza na vibaiskeli mnawapatia hela wanachukua wao wanaweka mfukoni, jioni wanampatia yule elfu 5 au elfu 3 halafu hela waliyopewa wanaondoka nayo”
“Kwahiyo ulemavu sasa ni mtaji, wanakwenda kuwasaka huko vijijini, kwanini nasema haya?, Mheshimiwa Rais ameboresha mazingira ya Walemavu na ukienda hapahapa Dar kuna kituo kikubwa cha kulelea Walemavu zaidi ya Tsh. trlioni 3 zimewekweza na Serikali kwenye vituo vingi Tanzania hatuna sababu ya kuwa na Watu wanaombaomba huko barabarani”