Aliyefariki apiga simu kuwatakia heri ya mwaka mpya ndugu zake



Familia ya Mzee Masengwa iliopo Kata ya Itenka Halmashauri Nsimbo mkoani Katavi imezua taharuki baada ya ndugu yao wanayedai alifariki dunia na kuzikwa kuonekana akiwa hai baada ya kupigia simu kuwatakia heri ya mwaka mpya.

Wakizungumzia tukio hilo ndugu wa marehemu wamesema walipigiwa simu ya kifo cha ndugu yao na rafiki zake aliokua akifanya nao kazi kisha kufika hospitali aliokua akipatiwa matibabu na kuonyeshwa mwili baada ya kuutambua walichukua na kwenda kuzika.

"Baada ya hiyo simu tulifika tukapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti ndugu yake huyu akaingia kuangalia mwili akatoka akasema ni yeye ila anasema mwili ulikua umeharibika sisi tukabeba kwenda kuzika. Siku ya mwaka mpya, Masanja aliyefariki akapiga simu kututakia heri ya mwaka mpya kwakweli tuliogopa sana tukasema amefufuka hatukuamini akasema mimi sijafa nilikua kijiji ambacho hakuna mtandao nilikua sipatikani," amesema shemeji yake Doto Shilinde.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Itenka, Misungwi Mikoba amesema familia hiyo ilizika mwili ambao sio wa ndugu yao huku akidai hakuna mtu aliefufuka katika kijiji chake kama inavyodaiwa.

Kwa sasa Masanja Masengwa aliedaiwa kufariki anaishi kwa mchungaji kwa lengo la kupumzika na kuwakimbia watu wanaotaka  kumuona  ili kujiridhisha kama ni yeye aliyepiga simu kwa ndugu zake. 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad