Aliyewahi kuwa Mbunge CHADEMA ahamia CCM

 


Aliyewahi kuwa mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa  Geita, Upendo Peneza, ametamgaza kujiengua na chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia sasa.


Peneza ametangaza uamuzi huo Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi.


"Nimeamua kujiunga na chama hiki kutokana na muelekeo mzuri unaofanywa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhu Hassan," Amesema Upendo


Aidha, Peneza amepingana na wito wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wa kuitisha maandamano ya kupinga muswada wa sheria za uchaguzi ambayo yamepangwa kufanyika Januari 24, mwaka huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad