Benchikha Achekelea vyuma Vilivyoshushwa Simba

 

Benchikha Achekelea vyuma Vilivyoshushwa Simba

Uongozi wa Simba SC umesema kocha wao Benchikha ameonekana kufurahishwa na michuano ya Kombe la Mapinduzi kwani imempa nafasi ya kujua mchezaji gani wa kubaki na wakuondoa yeye mwenyewe bila kuambiwa na mtu.


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema licha ya kutopata ubingwa, lakini kocha wao Benchikha ameonekana kuyafurahia mashindano hayo kwani ameshuhudia mwenyewe kwa macho yake viwango vya wachezaji wake wote, hivyo atafanya maamuzi yeye mwenyewe.


“Benchika amesema amepata muda mrefu wa kuwaona wachezaji wake na hasa wale ambao wamekuwa hawapati namba kwenye kikosi cha kwanza, ametuambia amemwona Luis Miqussone akirejea kwenye kiwango na pia amepata muda wa kumtazama Hussein Kazi akisema ni hazina, lakini amesema kuna wachezaji ambao hajaridhika nao na atawaacha.


“Hii yote ni kwa sababu ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, vinginevyo sijui ingekuwaje, kwa hiyo kaeni mkao wa kujua tukaoachana nao, tayari mwalimu amewapa nafasi baadhi ya wachezaji na amejiridhisha kuwa hawawezi kumsaidia kwenye safari yake huko mbele,” amesema Ahmed Ally

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad