Bondia Hassan Mwakinyo ameshinda pambano usiku huu kwa kumpiga Bondia wa Ghana Elvis kwa KO katika round ya 7 ya pambano hilo la kuwania ubingwa wa WBO Africa ambalo limepigwa New Amaan Complex Zanzibar.
Bondia Hassan Mwakinyo baada ya kumpiga Bondia wa Ghana Elvis kwa KO katika raundi ya 7 kwa mara nyingine ametuma salamu Morogoro (Kwa Twaha Kiduku) akisema hamuogopi na kama atatokea Promota wa kuweka dau kubwa yupo tayari kupigana nae hata pambano la kirafiki ili ajulikane nani ni Mbabe kati yao.
Mwakinyo amesema “Elvis sio Bondia rahisi na hajawahi kupoteza kwa KO hii ni ya mara yake ya kwanza na ni Bondia ambaye anacheza kilo 78 Mimi nimempandia uzito ni kiu changu cha muda mrefu lakini nilitaka kuwaprove WBO kwamba mwili wangu na uwezo nilionao ni vitu tofauti”
“Lakini pia nilikuwa nataka kutuma salamu Morogoro kwa Watu ambao walikuwa wanaamini naogopa zile piko kama Mabibi harusi wa huku , nilikuwa nataka kutumia hii fursa kama mfano wa kuonesha kwamba dau likifikwa ambalo lipo katika makubaliano yangu Mimi na Timu yangu pambano litapigwa hata la kirafiki ili tuone nani ni nani!?”