CHADEMA: Hatujawahi kimbia midahalo

 

CHADEMA: Hatujawahi kimbia midahalo

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kimesikia kauli ya ya Katibu wa Uenezi wa CCM, Paul Makonda akitoa rai kuwa anaomba ufanyike mdahalo baina ya Viongozi wa CHADEMA na yeye binafsi kabla ya maandamano yao waliyoyaitisha January 24,2024 ambapo CHADEMA wamesema wapo tayari na hawajawahi kukimbia midahalo.


Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema imesema mdahalo huo unaweza kufanyika katika masuala mbalimbalI ambayo CHADEMA imeweka msimamo wake wazi ili yatekelezwe na Serikali ikiwemo Serikali kuondoa kwanza miswada mitatu isiyofaa Bungeni ili kuwezesha Wadau mbalimbali kukaa kwenye mdahalo wa kujadili maudhui ya miswada ya sheria za uchaguzi, Tume ya Uchaguzi na Sheria zinazohusu maswala ya Vyama vya siasa.


“Serikali ianzishe mara moja mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Mwaka 1977 (Minimum reforms) ili kuwezesha kuondoa mapungufu yaliyopo kwenye Katiba hiyo ili kuruhusu maandalizi ya kuandikwa Kwa miswada mipya ya kuboresha mifumo ya chaguzi nchini na pia Serikali iwasilishe Bungeni muswada wa sheria ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi huo usimamiwe na Tume ya Uchaguzi badala ya TAMISEMI”


“Serikali iwasilishe Bungeni muswada wa Sheria wa kukwamua mechakato wa Katiba Mya ukiwa na mwelekeo (Road Map wa lini Nchi itapata Katiba Mpya) na pia Wadau tutaweza kukaa kwenye mdahalo ili kuishauri Serikali jinsi ya kuweza kupunguza ukali wa gharama za maisha na kuonyesha Kodi na tozo zipi zipunguzwe, anasa gani ziondolewe Serikalini na mkakati mzima wa kupunguza ukali wa gharama za maisha kwa Wananchi.


“Hivyo basi katika kipindi hiki aweke mdahalo na Serikali ili waone ulazima wa kusikiliza na kuheshimu maoni ya Wananchi na Wadau mbalimbali wa chaguzi katika kuandaa mazingira bora ya kuwa na chaguzi huru na haki nchini, katika kipindi hiki Chama kinaendelea na maandalizi ya maandamano ya amani yatakayofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 24 Januari, 2024”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad