CHADEMA: TAMISEMI isimamishe Uchaguzi Serikali za Mitaa

 

CHADEMA: TAMISEMI isimamishe Uchaguzi Serikali za Mitaa

Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeazimia Serikali iwasilishe muswada Bungeni ambapo pamoja na mambo mengine Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipewe Mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na sio kusimamiwa na TAMISEMI kwa kanuni ambazo zinatungwa na Waziri.


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza maazimio hayo leo January 13,2024 Jijini Dar es salaam ambapo pia amesema Kamati Kuu ya CHADEMA imeazimia kuwa miswada iliyowasilishwa Bungeni November 10,2023 iondolewe Bungeni na badala yake Serikali iwasilishwe muswada Bungeni wa kukwamua mchakato wa Katiba mpya pamoja na mwelekeo kwa kila hatua mpaka ipatikane Katiba mpya itakayopatikana kwa kuzingatia mwafaka wa Kitaifa.


“Tumeazimia pia Serikali iwasilishe Bungeni muswada wa kufanya marekebisho ya mpito ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ili uchaguzi uwe huru na haki baada ya kuondoa mapungufu ya kisheria yaliyopo sasa “


“Muswada wa marekebisho ya sheria za Vyama vya Siasa, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, uondolewe kwakuwa haujazingatia amri ya Mahakama ya Afrika Mashariki kwasababu baadhi ya vifungu viliambiwa vinakiuka mkataba wenyewe wa Afrika Mashariki”


“Miswada iliyowasilishwa Bungeni November 10,2023 iondolewe na kuandikwa upya, Dodoma kuna Bunge lakini kimsingi ni Bunge la Chama kimoja, walewale wanaoharamisha uchaguzi na mifumo yetu ya haki eti ndio wao watutungie sheria wanavyotaka wao , uwezekano ni kidogo sana kwa Bunge la Dodoma kufanya maamuzi ambayo yatatenda haki kwa wote, kwahiyo CHADEMA tunaamini kama Serikali ingekuwa na nia ya kufanya mabadiliko ya kweli hata maoni yaliyokusanywa kwa miaka miwili yangetosha kutafuta mwafaka wa Kitaifa”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad