CHADEMA Yaitisha Maandamano Januari 24

CHADEMA yaitisha maandamano Januari 24


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza maandamano ya amani ya kuishinikiza Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya Wadau mbalimbali wa Uchaguzi nchini kuhusu kuwa na Tume Huru itakayosimamia Uchaguzi kwa haki, ambapo maandamano hayo yataanza Dar es salaam kuanzia January 24,2024.


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza uamuzi huo leo Jijini Dar es salaam ambapo amenukuliwa akisema “Kamati Kuu ya CHADEMA imeazimia ni kwamba kwakuwa mapendekezo yetu yote yameonekana kukataliwa, Chama kimatangaza maandamano ya amani ya kuishinikiza Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya Wadau mbalimbali wa Uchaguzi nchini ambayo yataanza Dar es salaam kuanzia January 24,2024 siku ya Jumatano na kuendelea Mikoani kwa jinsi itakavyopangwa mpaka pale Serikali itakapoondoa miswada hiyo na kusikiliza maoni na kuheshimu maoni ya Watanzania”


“Baba wa Taifa Mwl. Nyerere amezungumza mengi kwa nyakati tofauti ikiwemo umuhimu wa kuheshimu maoni ya Wananchi, wenzetu hawamuheshimu hata Mwasisi wa Chama chao, Tanzania ni yetu sote na hatuna budi kuilinda”


“Mimi nilikuwa Mtetezi mkubwa wa maridhiano kwasababu niliamini maridhiano ni msingi mzuri wa ujenzi wa Taifa na hata wenzangu waliponitaka nitoke kwenye maridhiano bado niliamini kwenye nafasi ya maridhiano lakini sasa nimejiridhisha bila uoga, hawa Watu wanapuuza maoni ya Wananchi, sasa hapo Mbowe nifanyaje?, ni lazima nikubaliane na wenzangu”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad