Chadema Yamjibu PAUL Makonda Kuhusu Maandamano





CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kiko tayari kufanya mdahalo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, endapo Serikali itafanyia kazi madai yao juu ya upatikanaji tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam..(endelea).

Msimamo huo umetolewa leo tarehe 15 Januari 2022 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema siku moja baada ya Makonda kutaka mdahalo na viongozi wa chama hicho.

“Msimamo wa chama ni kuwa, kama anataka mdahalo na sisi kama chama tupo tayari na hatujawahi kukimbia midahalo kama wao na chama chao. Hivyo basi, mdahalo unaweza kufanyika katika masuala yafuatayo ambayo tumeweka msimamo wetu wazi ili yatekelezwe na Serikali,” imesema taarifa ya Mrema.

Taarifa ya Mrema imetaja mambo hayo kuwa ni Serikali kuondoa bungeni miswada mitatu ya marekebisho ya sheria za uchaguzi ambayo Chadema inadai kuwa mibovu. Serikali ianzishe mara moja mchakato wa marekebisho ya katiba ya 1977 ili kuwezesha kuondoa mapungufu yaliyopo kwenye katiba hiyo ili kuruhusu maandalizi ya kuandikwa miswada mipya ya kuboresha mifumo ya ucvhaguzi.

Aidha, kupitia taarifa hiyo Mrema amesema mpango wa Chadema kufanya maandamano yasiyo na kikomo kuanzia tarehe 24 Januari mwaka huu, hadi Serikali itakapofanyia kazi madai yao, uko palepale.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad