Danadana Treni ya SGR: Rais Samia Avunja Ukimya




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Mamlaka zinazohusika na usafirishaji Nchini kuhakikisha Julai 2024 safari za Treni ya mwendo kasi inaaza rasmi kutoka jiji la Dar es salaam hadi Makao Makuu ya nchi, Dodoma.

Rais Samia ameyasema hayo katika salam zake za Mwaka mpya alizozitoa kupitia Hotuba yake na kudai kuwa Wananchi wamechoshwa kusikia mara kadhaa kwamba safari bado zinaahirishwa.

Amesema, “nimekuwa nikisia mabadiliko ya tarehe ya kuanza kwa safari za treni kupitia Reli ya mwendo kasi-SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na kwa kweli wananchi wamechoshwa na vijisababu wanataka kuona reli ikifanya kazi na sasa nielekeze ifikapo mwisho wa mwezi July 2024 safari ya Reli ya SGR kati ya Dar es Salaam hadi Dodoma ziwe zimeanza.”

Katika Salamu zake za mwaka mpya kwa Taifa ambayo imejikita zaidi katika mapito ya mwaka unaisha wa 2023, pia amekiri kuwepo kwa changamoto kadhaa za upatikanikaji wa umeme na kuahidi kuwa Serikali inalifanyia kazi jambo hilo.

Aidha, amebainisha kuwa vipande vya Reli hiyo vya kutoka Dar es Salaam, Morogoro hadi Makutupora zimefikia zaidi ya asilimia 90.

Amesema, Serikali imepata udhamini wa Benki ya Maendeleo ya Afrika utakaowezesha uendelezaji wa kipande cha Tabora- kigoma na Uvinza Msongati.

Hata hivyo, hotuba yake ambayo iliangazia mafanikio ya mwaka 2023 na kutoa mwelekeo wa mwaka 2024 pia ulitumika kuwahamasisha Wananchi kujitokeza na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kuanza mwaka ujao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad