"Ndio maana mimi huwa nina maamuzi yangu magumu, mimi mwanaume aniambie nageuka kuwa mchepuko halafu mchepuko ndio anakuwa mke!! si aliongea kwenye kipindi cha radio, muda huohuo akirudi nyumbani anakuta nimekusanya mabegi yangu nimeondoka. Yule mke wake hana pakwenda na hii inatokana na uvivu wake wa kutokufanya kazi, fanyeni kazi wanawake ili wanaume zenu wawaheshimu"- Dida Shaibu
Didah ambaye ni mtangazaji maarufu muda mrefu, pia amekuwa mfanyabisha kwa miaka mingi ikiwemo duka la nguo na amejenga. Alishaolewa katika ndoa nne na wanaume waliokuwa na kazi nzuri , wengine wafanyabishara wenye majina lakini yeye ndie mara zote ameelezwa kuzikimbia ndoa husika bila kupoteza muda mrefu sababu kubwa akizitaja ni kukataa unyanyasaji na udhalilishaji ndani ya ndoq, huku moja ya mambo ya aibu yanayodaiwa ndio aliyakimbia kutoka kwa mmoja wa wanaume waliowahi kumuoa yakitajwa mitandaoni