Drogba asema Ivory Coast kuna shida




ABIDJAN, IVORY COAST. DIDIER Drogba amekiri Ivory Coast kuwa kwenye matatizo makubwa baada ya kushindwa kufuzu hatua ya mtoano ya 16 bora kwenye fainali za Afcon 2023 kwa nguvu yao na kubakia kuomba dua tu.

Ivory Coast, ambao ni wenyeji wa fainali za Afcon 2023 juzi Jumatatu walikumbana na kipigo cha kudhalilisha kutoka kwa Equatorial Guinea baada ya kuchapwa 4-0 kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Ebimpe.

Kipigo hicho kimefanya kikosi hicho cha Tembo kumaliza Kundi A kwenye nafasi ya tatu, wakisubiri majaliwa yao ya kufuzu hatua ya 16 kwa kigezo cha timu ya tatu bora kama tu Cameroon itakuwa haijapata ushindi dhidi ya Gambia katika mchezo wa usiku wa jana Jumanne.

Mashabiki wa Ivory Coast walichukizwa na wachezaji wao baada ya kipigo hicho cha Equatorial Guinea na vikosi vyote vilizuiwa kutoka uwanjani kwa sababu za kiusalama.

Drogba, ambaye alikuwa nahodha wa Ivory Coast wakati akiwa mchezaji na ambaye hadi sasa bado anashikilia rekodi ya kuwa kinara wa mabao wa muda wote, hakutaka kuficha mambo baada ya kipigo hicho kutoka kwa Equatorial Guinea.

"Yatupasa kurudi kazini na si tu kujiuliza maswali magumu, bali kufanya uamuzi sahihi pia," alisema Drogba na kuongeza. "Ni kwa ajili ya soka, kwa sababu nchi kama Ivory Coast haiwezi kuandaa fainali za Afcon kisha ikatolewa mapema. Kuna tatizo kubwa."

Kocha wa Ivory Coast, Jean-Louis Gasset alisema wachezaji wake waliangua vilio kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kipigo hicho, akisema: "Ni majanga."


"Tuliajiandaa vizuri kwa ile mechi. Tulimiliki mpira na kutengeneza nafasi. Tulikuwa tunalazimisha mambo na hatufungi mabao. Kwenye soka unapaswa kuwa sahihi sana. Equatorial Guinea imetupa somo."

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad