Mwanamuziki wa singeli nchini, Dulla Makabila, ameendelea kujipakulia minyama kutokana na wimbo wake uitwao 'Furahi' kukamatia namba moja kwenye mtandao wa YouTube kwa zaidi ya siku tatu mfululizo.
Wimbo huoulishika namba moja kwenye mtandao huo kabla ya saa 20 jambo ambalo linamfanya aendelee kuvimba na sasa anajiita mfalme wa singeli.
Kupitia mtandao wa Instagram msanii huyu ameshusha ujumbe akieleza kuwa yeye ndiye mfalme wa muziki huo kwa sasa, kwa sababu tangu dunia ianze wimbo wake ndiyo wa kwanza kwenye upande wa singeli kuingia ‘trending’ namba moja kabla ya saa 20.
Hata hivyo, Makabila amewataka wasanii wengine kujifunza kutoka kwake kwani anaamini kuwa maendeleo hayana chama. “Hadi sasa 'Furahi' bado upo namba moja YouTube umefikisha 624k huku ukiwa na siku sita tu tangu utoke”.
Ikumbukwe kuwa wimbo huo ndiyo ulisababisha Januari 24, 2024 Makabila kutakiwa 'kuripoti' Kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya mahojiano, baada ya kudaiwa mistari yake inamlenga aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara na mkewe Zaiylissa, ambaye awali alikuwa mke wa Makabila