Gamondi Awasilisha Ombi Moja Young Africans




Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amewaambia mabosi wa timu hiyo wafanye kila wanaloweza apate mchezo wa kimataifa wa kirafiki kabla ya kurejea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya mapunziko ya kupisha michuano ya AFCON 2023 kumalizika.

Gamondi ametoa kauli hiyo kufuatia kuendelca na programu za mazoezi na wachezaji wake wote ambao hajaitwa kwenye timu za taifa zinazoshirilki AFCON 2023.

Mbali na bapo Gamondi anataka kumpima Mshambuliaji wao mpya, Joseph Guede ambaye amesajiliwa kwenye dirisha hili dogo na ndiye atakuwa straika kiongozi kwenye kikosi cha Young Africans.

Imefahamika kuwa, kocha huyo ameuomba uongozi wake michezo miwili ya kirafiki kwa ajili ya kuwapa mechi fitinesi nyota wake.

Gamondi amesema kuwa kuna kila sababu ya timu yake kupata michezo ya kimataifa ya kirafiki wakati huu wa mapumziko ili kujua ubora wa kikosi chake kwa kupata muunganiko ukiwemo wa wachezaji wapya kabla ya kurejea kwenye michuano ya kimataifa.

“Tunaendelea na mipango yetu kwa sababu bado kazi kubwa ipo mbele yetu na ukiangalia wachezaji baadhi walikuwa kwenye mapumziko mafupi hawakuwepo katika Kombe la Mapinduzi, hivyo tumerejea mapema kuweza kujipanga kwa muda huu ambao upo kwa sasa, lakini wapo wapya ambao wameingia wanahitaji kuzoea timu ili tufikie malengo.

Lazima tucheze mechi za kirafiki hasa upunde wa kimataifa wakati huu ligi imesimama, ikiwezekaa na nyengine za ndani kwa ababu tunalenga kuboresha timu yetu kwa malengo ya kufanya vizuri kimataifa na wachezaji waliongia waweze kwenda sawa na waliokuwepo” amesema Gamondi.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad