Haya Ndio Mafanikio ya Simba Wanayojivunia



Haya Ndio Mafanikio ya Simba Wanayojivunia


“Tunataka kuwa mabingwa wa ndani na nje ya uwanja. Tulianzisha WhatsApp channel wakawa wanatusema lakini leo hii tunaongoza kwa kuwa namba moja Afrika Mashariki na Kati na walikuwa wametuzidi YouTube lakini hivi ninapoongea sasa tumewapita na tunaongoza kwenye mitandao yote.”

“Tutaendelea kujenga rasilimali za Simba na eneo lingine ni kuwa na wafanyakazi wenye weledi na uwezo mkubwa sana. Mbele tunaangalia kuboresha mapato, kuimarisha biashara ya jezi.”

“Sandaland amefanya yale mliyokuwa mnayataka kama jezi kutoka mapema na jezi yenye ubora. Ni mzabuni aliyetimiza malengo yenu wanachama. Mwaka huu tunaangalia namna ya kushirikisha matawi katika uuzaji wa jezi ili kuwaongezea mapato.”

“Changamoto zilizopo ni rasilimali fedha, kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, kutanuka kwa mahitaji, kuumia kwa wachezaji, mabadiliko na ushindani kuongezeka na kuendelea kuwa timu namba moja.”- CEO Imani Kajula.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad