Hivi Ndivyo Haji Manara Amvalisha Pete ya Uchumba Zaylissa

Haji Manara Amvalisha Pete ya Uchumba Zaylissa


Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara amvisha pete ya uchumba mpenzi wake Zaylissa siku ya jana Januari 18, 2024


Sherehe hiyo ya kuvishana pete ilienda sambamba na kusherehekea kumbukizi ya siku ya  kuzaliwa Haji, ambapo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Aunty Ezekiel, Arene Uwoya, Diamond, Lamata, Nandy na  Ommy Dimpoz.


Katika sherehe hiyo Haji ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa anaomba sana dua za mashabiki wake  kwani anatamani ndoa anayotarajia kufunga na Zay iwe ya mwisho kwake.


Zay na Haji walianza kuhusishwa kwenye uhusiano wa kimapenzi mapema Novemba mwaka jana, ingawa mwanzo waligoma na kudai kuwa wapo kwenye urafiki wa kawaida.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad